Andy García
| Andy Garcia | |
Garcia mwaka 2026 | |
| Amezaliwa | 12 Aprili 1956[1] Havana, Kuba[1] |
|---|---|
| Nchi | Marekani |
| Elimu | Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Florida[2] |
| Urefu | 175 cm |
| Kipindi | 1978–sasa |
| Watoto | 4 (akiwemo Dominik García-Lorido) |
Andrés Arturo García Menéndez (alizaliwa Aprili 12, 1956) ni mwigizaji, muongozaji, mtayarishaji, na mwanamuziki wa Marekani. Alianza kupata umaarufu mkubwa kwa kuigiza katika filamu ya Brian De Palma iliyoitwa The Untouchables (1987) akishirikiana na Kevin Costner, Sean Connery, na Robert De Niro. Aliendelea kuigiza katika filamu kama vile Stand and Deliver (1988), na Internal Affairs (1990). Baadaye alishiriki katika filamu ya Francis Ford Coppola ya The Godfather Part III (1990) kama Vincent Mancini, jambo lililomwezesha kuchaguliwa kuwania Tuzo ya Akademi (kama mwigizaji bora wa kiume anayesaidia) na kuwa mwigizaji wa kwanza kutoka Kuba kuchaguliwa kuwania tuzo za Oscar katika kategoria ya uigizaji.
Aliendelea kuigiza katika filamu za Hollywood kama vile filamu ya Stephen Frears ya Hero (1992), filamu ya vichekesho na mapenzi ya When a Man Loves a Woman (1994), na filamu ya mapambano na kusisimua ya Desperate Measures (1998). Mnamo mwaka 2000, alitayarisha na kuigiza katika filamu ya televisheni ya HBO iliyoitwa For Love or Country: The Arturo Sandoval Story (2000), ambapo alichaguliwa kuwania Tuzo ya Primetime Emmy Award na Tuzo ya Golden Globe Award. Pia, alicheza katika filamu ya Steven Soderbergh ya Ocean's Eleven (2001) na muendelezo wake wa Ocean's Twelve (2004) na Ocean's Thirteen (2007). Mnamo mwaka 2005, Garcia aliongoza na kuigiza katika filamu ya The Lost City akishirikiana na Dustin Hoffman na Bill Murray. Alishiriki pia katika New York, I Love You (2008), filamu ya vichekesho na drama ya City Island (2009), filamu ya vichekesho na mapenzi ya At Middleton (2013), na filamu ya kusisimua ya makosa ya jinai ya Kill the Messenger (2014). Ameshika nafasi za usaidizi katika filamu za Mamma Mia! Here We Go Again, Book Club, The Mule, filamu ya televisheni ya HBO ya My Dinner with Hervé (zote za mwaka 2018), na kucheza uhusika mkuu katika toleo jipya la filamu ya Father of the Bride (2022).
Mnamo mwaka 2005, alishinda Tuzo ya Grammy na Tuzo ya Latin Grammy kwa kutayarisha rekodi ya mwanamuziki wa Kuba Cachao iliyoitwa ¡Ahora Sí!.[3][4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 "Andy Garcia Biography". Biography.com (FYI/A&E Networks). Iliwekwa mnamo Mei 17, 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Andy Garcia: Biography". Net Glimpse. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Desemba 5, 2004. Iliwekwa mnamo Desemba 19, 2010.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Andy Garcia". The Recording Academy. Iliwekwa mnamo 2024-05-31.
- ↑ "Andy García". The Latin Recording Academy. Iliwekwa mnamo 2024-05-31.